Connect with us

General News

Tundo afungua pengo la alama 27 msimamo wa Mbio za Magari Afrika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na GEOFFREY ANENE

DEREVA Mkenya Carl “Flash” Tundo amefungua mwanya wa alama 27 juu ya jedwali la Mbio za Magari za Afrika (ARC) baada ya kuzoa ushindi wake wa tatu mfululizo msimu huu wa 2021 kwa kutawala Sarago Zambia Rally nchini Zambia mnamo Septemba 24-26.

Tundo, 48, ambaye alikamilisha Zambia Rally katika nafasi ya tano mwaka 2019, ana jumla ya alama 90 msimu huu akishirikiana na mwelekezi wake Tim Jessop katika gari la Volkswagen Polo R5.

Aliwasili nchini Zambia akifurahia mataji ya duru za Equator Rally katika maeneo ya Naivasha mwezi Aprili na duru ya Oryx Energies nchini Tanzania mwezi Agosti.Bingwa huyo mara tano wa Safari Rally ya Kenya mwaka 2007, 2009, 2012 na 2018, anafuatiwa kwa karibu na Guy Botterill aliye na alama 73.

Botterill alikamata nafasi ya 14 kwenye duru ya ufunguzi ya Bandama nchini Ivory Coast mwezi Februari.Botteril hakupata alama nchini Ivory Coast pia Equator Rally kwa kukamilisha mbio akiwa amechelewa sana baada ya gari lake kukumbwa na hitilafu.

Alikamata nafasi ya nne nchini Tanzania kabla ya kuwa nambari mbili nchini Zambia. Dereva huyo mwenye umri wa miaka 34 anaendesha gari la Toyota Etios akishirikiana na Simon Vacy-Lyle.

Tundo afungua pengo la alama 27 msimamo wa Mbio za Magari Afrika – Taifa Leo
PICHA/GEOFFREY ANENE

Mganda Yasin Nasser, ambaye anaelekezwa na Ali Katumba katika gari la Subaru Impreza, anafunga mduara wa tatu-bora kwa alama 49.Tundo ni Mkenya wa tatu kutwaa ubingwa wa Zambia Rally baada ya Manvir Baryan mwaka 2017, 2018 na 2019 na Jaspreet Chatthe (2015).

Amejiweka pazuri kufuata nyayo za bingwa wa Afrika, Manvir. Duru ijayo itaandaliwa nchini Rwanda mnamo Oktoba 22-24 kabla ya msimu kufikia kilele nchini Afrika Kusini mnamo Novemba 26-27.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending