Connect with us

General News

Turuhusiwe kuagiza mahindi kutoka nje – Kampuni za unga – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Turuhusiwe kuagiza mahindi kutoka nje – Kampuni za unga – Taifa Leo

Turuhusiwe kuagiza mahindi kutoka nje – Kampuni za unga

NA BARNABAS BII

VIWANDA vya unga sasa vinataka viruhusiwe kuagiza magunia milioni 4 kutoka nje ili kunusuru zaidi ya Wakenya milioni 3 wanaohangaishwa na njaa nchini.

Chama cha Watengenezaji wa Unga cha Grain Belt (GBMA), kinasema kuwa viwanda vingi vimesitisha shughuli kutokana na ukosefu wa mahindi.

“Kampuni zaidi ya 10 tayari zimelazimisha wafanyakazi wao kwenda likizoni kutokana na ukosefu wa kazi uliosababishwa na uhaba wa mahindi,” akasema Bw Kipngetich Mutai, mwenyekiti wa GBMA.

Alisema kuwa viwanda vingi vimekuwa vikisaga kiasi kidogo cha mahindi kuliko

kawaida ndani ya wiki mbili zilizopita.

Kulingana na Bw Mutai bei ya mahindi imepanda kutoka Sh3,400 hadi Sh3,650 kwa kila gunia la kilo 90.

“Tutakutana na maafisa wakuu kati – ka wizara ya Kilimo ili waturuhusu kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi,” akasema Bw Mutai.

Alisema kuwa viwanda vya Kaunti za Bungoma, Busia, Kisumu, Narok, Kajiado na vingine vinne katika eneo la Mlima

Kenya ndivyo vimeathiriwa zaidi na uhaba wa mahindi.

Uhaba wa mahindi unaoshuhudiwa nchini umesababisha na mavuno duni ya zao hilo msimu uliopita na ongezeko la wafanyabiashara wakora ambao wameficha mahindi.

“Viwanda vingi katika maeneo ya Eldoret, Moi’s Brigde na Kitale vimeishiwa na mahindi na huenda vikasitisha shughuli ndani ya siku chache zijazo,” akasema Bw David Kosgei, mfanyakazi wa kiwanda cha unga mjini Eldoret.

Pakiti moja ya kilo mbili za unga wa mahindi sasa inauzwa kwa Sh115 katika maduka mengi ya magharibi mwa Kenya badala ya Sh80.

Bw Mutai anaonya kuwa kampuni za unga huenda zikapandisha bei ya bidhaa hiyo kufuatia ongezeko la bei ya mahindi.

“Wateja ndio watahisi makali ya bei ya juu ya unga kwani sisi hatutakubali kupata hasara,” akasema.

Wizara ya Kilimo imeshikilia kuwa nchi ina mahindi ya kutosha ya kulisha nchi hadi mwishoni mwa Aprili.

Kampuni za unga zinataka serikali iondoe vikwazo kuwezesha mahindi kutoka nchi jirani kuingizwa nchini.

Wanasema hatua hiyo itasaidia kupungua kwa bei ya mahindi hivyo kukinga wateja dhidi ya bei ya juu.

Wakulima wengi katika eneo la Bonde la Ufa wameficha mahindi huku wakin – gojea bei kuongezeka kabla ya kuyauza.

Uchunguzi wa Taifa Leo umebaini kuwa kampuni kubwa za unga kama vile Mombasa Millers, Unga, Pembe, Dola na Kitui pia zinakabiliwa na wakati mgumu kupata mahindi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending