Connect with us

General News

Ubidhaaishaji wa Kiswahili katika mfumo wa kiumilisi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ubidhaaishaji wa Kiswahili katika mfumo wa kiumilisi – Taifa Leo

NGUVU ZA HOJA: Ubidhaaishaji wa Kiswahili katika mfumo wa kiumilisi

NA PROF JOHN KOBIA

MFUMO wa elimu wa Umilisi unaondelea kutekeleza nchini Kenya umekipa Kiswahili nafasi mwafaka ya kuwa bidhaa.

Bidhaa ni kitu kinachonunuliwa na kuuzwa. Kiswahili ni raslimali muhimu tunayouza na ikanunuliwa nchini Kenya, barani Afrika na kwingineko duniani. Kama raslimali yoyote, ile lazima ilindwe na kutunzwa ipasavyo.

Katika mfumo wa umilisi, Kiswahili ni bidhaa muhimu kwa watakaohitimu katika daraja mbalimbali. Katika daraja ya awali ya shule za upili, wanafunzi wanatarajiwa kukuza umilisi wa kutunga nyimbo nyepesi mbalimbali kama bembelezi, nyimbo za watoto, za kazi na za dini. Umilisi huu utaimarisha talanta zao na kuwa waimbaji wa nyimbo. Wanatarajiwa kuwasilisha nyimbo walizotunga kwa kutumia mitindo mbalimbali. Wanapoimba nyimbo kwa kutumia Kiswahili na kuzirekodi kwenye sidii na kuziuza, Kiswahili kinatumiwa kama bidhaa muhimu.

Wanafunzi wanapata umilisi wa kusoma habari kwa ufasaha kwa kuzingatia matamshi sahihi, kusoma kwa kasi ifaayo na kuambatanisha ishara katika usomaji. Umilisi huu unawaandaa kuwa wasomaji na watangaziji wa habari katika redio au televisheni.

Kuna vituo vingi vya utangazaji vya redio na televisheni ambavyo hutangaza kwa Kiswahili. Wanapopata ajira katika vituo hivi, Kiswahili hutumiwa kama bidhaa.

Stadi ya kuandika kwa Kiswahili inakuzwa kupitia kuandika kwa kazi za kibunifu, muhtasari, hotuba, barua za aina mbalimbali na uhariri.

Kiswahili ni bidhaa muhimu kwa sababu kuandika hotuba ni taaluma yenye tija katika mawasiliano. Vilevile, kuandika kazi za kibunifu kama vile novela ni njia ya kubidhaaisha Kiswahili.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending