Connect with us

General News

UDA yatangaza tarehe za mchujo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

UDA yatangaza tarehe za mchujo – Taifa Leo

UDA yatangaza tarehe za mchujo

 Na CHARLES WASONGA

CHAMA cha United Democratic Alliance (UDA) kimetangaza kuwa kitaendesha mchujo wa wagombeaji nyadhifa mbalimbali kwa tiketi ya chama hicho kati ya Aprili 9 na 16 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi (NEB) wa chama hicho Jumatano, Februari 16, 2022 Anthony Mwaura kwa mara nyingine aliwahakikishia wagombeaji wote kwamba hakuna wawaniaji wanaopendelewa na kwamba chama hicho hakitatoa tiketi ya moja kwa moja kwa yeyote.

“Naibu Rais William Ruto ametoa hakikisho kwamba mchujo utaendeshwa kwa njia huru na haki. Wanjiku ndio ataruhusiwa kuamua wagombeaji ambao watapeperusha bendera ya UDA katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9,” Bw Mwaura akasema kwenye taarifa.

Mwenyekiti huyo aliongea kuwa chama hicho kinafanya mazungumzo na washirika wake katika muungano wa Kenya Kwanza kwa nia ya kufanya mchujo wa pamoja.

“Aidha, katika maeneo mengine huenda mfumo wa kura ya maoni ukatumiwa kubaini wawaniaji ambao ni maarufu zaidi katika maeneo husika,” Bw Maura akasema.

Kulingana na mwenyekiti huyo chama hicho kinachoongozwa na Dkt Ruto kimeanzisha mchakato wa kuthibitisha wawaniaji ambao wamelipa ada za uteuzi.

Kwenye tangazo lilichapishwa katika vyombo vya habari mapema mwezi huu, wale wote wanaotaka kuwania viti mbalimbali katika uchaguzi wa Agosti 9, 2022 walipewa muda wa hadi Februari 28, 2022 kuipa ada hizo.

Kulingana na tangazo hilo, wale wanaomezea mate kiti cha urais wanahitaji kulipa Sh1 milioni huku wanawake na vijana wakilipa Sh500,000

Wanaume wanaotaka tiketi ya kuwania ugavana nao watahitajika kulipa ada ya Sh500,000 huku wanawake na vijana wakilipa Sh250,000.

Wanataka tiketi za kuwania nyadhifa za Wawakilishi wa Kike katika Kaunti watahitajika kulipa Sh250,000 huku vijana wakitoa Sh125,000.

Wanaomezea mate viti vya ubunge nao watalipa Sh250,000 sawa na maseneta huku vijana wakilipa Sh125,000.

Kwa upande wa viti vya udiwani, ada ya uteuzi ni Sh50,000 kwa wanaume na Sh25,000 kwa vijana na wanawake.

Watu wanaoishi na aina yoyote ya ulemavu hawatahitajika kulipa ada zozote za uteuzi endapo wangetaka kuwania nyadhifa hizo zote kwa tiketi ya chama cha UDA.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending