Connect with us

General News

Ulikosea stepu, Ruto amwambia Uhuru – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ulikosea stepu, Ruto amwambia Uhuru – Taifa Leo

Ulikosea stepu, Ruto amwambia Uhuru

Na CHARLES WASONGA

NAIBU Rais William Ruto, na wandani wake, wamemjibu Rais Uhuru Kenyatta ambaye amemlaumu (Ruto) kwa kutosaidia katika kushughulikia tatizo la kupanda kwa gharama ya maisha nchini.

Akiongea katika sherehe za Leba Dei katika Uwanja wa Nyayo Jumapili, Mei 1, 2022, Rais Kenyatta amemlaumu Ruto kwa kudai kuwa yeye (rais) ndiye chimbuko la tatizo hilo.

Lakini akimjibu muda mfupi baadaye, Dkt Ruto ameelekeza kidole cha lawama kwa Rais Kenyatta akisema ni yeye (rais) aliyempokonya majukumu na kuwapa watu wengine.

“Ninahisi uchungu wako. Wale ambao uliwapa majukumu yangu na mzee mradi wako, wamefeli kabisa,” Dkt Ruto akasema.

“Walivuruga Ajenda Nne Kuu, wakaua chama chetu na wakaharibu muhula wako wa pili. Bosi, ninapatikana haraka kwa njia ya simu. Inasikitisha kuwa kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri kilifanyika miaka miwili iliyopita,” Dkt Ruto akasema kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Dkt Ruto amesema hayo dakika chache baada ya Rais Kenyatta kusema kuwa yeye (Dkt Ruto) na wandani wake wamekuwa wakiwapotosha Wakenya kuhusu chimbuko la kupanda kwa gharama ya maisha.

Rais amejitetea akidai kuwa serikali yake imefanya mengi kuwakinga Wakenya dhidi ya makali ya ugumu wa kiuchumi yaliyosababishwa na janga la Covid-19 na hatua ya Urusi kuvamia Ukraine mnamo Februari 24, 2022.

Rais Kenyatta alisema kuwa serikali yake imefanya mengi kuwapunguzia Wakenya mzigo wa kupanda kwa gharama ya maisha licha ya Dkt Ruto kutelekeza majukumu yake badala ya kutoa suluhu.

“Sio Wakenya walioleta janga la Covid-19 ambalo lilichangia watu kupoteza nafasi za ajira. Kupanda kwa gharama ya maisha kumesababishwa pia na vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Hizi ni sababu ambazo zimezidi uwezo wetu,” Rais akasema.

“Badala ya kuja kunisaidia kwa kutoa ushauri wako, wewe unatumia muda wako mwingi kunitusi katika masoko. Hii ni licha ya kwamba unajiita kuwa kiongozi wa cheo cha juu serikalini; eti wewe ni nambari fulani.

“Ungeondoka kitambo ili nitafute mtu mwingine ambaye anaweza kunisaidia kufanya kazi,” Rais Kenyatta akasema.

Nao wafuasi wa Dkt Ruto wamemkaripia rais wakisema anasikitika kwa kumtenda naibu wake, pamoja na wandani wake.

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amemkumbusha Rais Kenyatta kwamba mnamo 2019 ni yeye alimvua Dkt Ruto majukumu yake kupitia Amri ya Urais Nambari 1.

“Hii ndio maana sasa umechanganyikiwa na kukosa mwelekeo. Wewe ndiwe unafaa kujilaumu,” Bw Murkomen akasema.

Naye Seneta Maalum Millicent Omanga akasema: “Huwezi kuzini kisha utarajie mkeo kutoibua malalamishi. Nyumba ndogo iliharibu ndoa.”

Bi Omanga alikuwa akirejelea hatua ya Rais Kenyatta kumtelekeza Dkt Ruto kupitia handisheki kati yake na kiongozi wa ODM Raila Odinga mnamo Machi 9, 2018.

Kwa upande wake aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Nchini (LSK) Nelson Havi amesema kuwa Rais Kenyatta hana sifa za kiongozi.

“Kiongozi anafaa kuongoza kwa haki na mke wa mfalme ataongoza kwa hukumu – Isaiah 32: 1. Ewe Rais Kenyatta huna sifa hizi,” akasema Havi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending