Akizungumza na wanahabari Jumatano, Julai 8, Macharia alisema treni ya kwanza itaondoka jijini Nairobi saa mbili asubuhi na itatarajiwa kufika Mombasa majira ya saa sita na dakika 45 mchana.
Treni hiyo vile vile itaondoka Mombasa saa saba na dakika 25 na inatarajiwa kufika Nairobi mwendo wa saa kumi na mbili na dakika 40, saa ambazo zitawawezesha abiria kufika makwao kabla ya kafyu kuanza.
Macharia alisema maafisa 10 watakuwa kwenye treni hiyo wakiwaelekeza abiria jinsi ya kuzingatia amri ya kutokaribiana.