Mwathiriwa mmoja ni Balozi wa Sudan Kusini, Washington Gordon Buay ambaye aliwaacha wenzake vinywa wazi na vicheko baada ya kujisaidia mbele ya watumizi watano wa Zoom.
Buay alikuwa anamsikiliza kwa makini mmoja wao wakati alihisi kubanwa na alionekana akielekea bafuni bila kuvalia chochote ila shati nyeupe.
Wakati huo, waliokuwa wamehudhuria walikuwa na sintofahamu ya namna balozi huyo alianika uchi wake akiwa katika mkutano muhimu.
“Nafikiri wahitaji kumzima Balozi Gordon Bouy, naamini ni yeye ndiye anapiga kelele,” alisema mmoja wa waliohudhuria.
Kabla ya wao kung’amua kile balozi huyo alikuwa anafanya, walimuona akianza kuenda haja ndogo huku ametazama kamera mbele ya wageni watano waliokuwa wamehudhurua mkutano huo.
Huenda kamera yake iliamua kumuanika huku akijaribu kufuatilia kile ambacho kilikuwa kinazungumziwa.
Wengi wa waliohudhuria mkutano huo waligutuka na kushikilia pumzi yao kwa muda, huku wengine wakiangua kicheko na kumpelekea kiongozi wa mkutano huo kukimbia kumfurusha mkutanoni.
Lakini tayari alikuwa amezua kioja.
Video hiyo ilizua msisimko kwenye mtandao jamii huku wengi wakishikilia kwamba alikuwa mlevi na kupelekea kupotoka kinidhamu.
Hii hapa baadhi ya maoni ya wanamtandao kwenye Facebook
Hata hivyo, balozi huyo si wa kwanza kujiaibisha kupitia mkutano mtandaoni.
Awali, TUKO.co.ke iliripoti kuhusu mwanamke mmoja ambaye aliwachwa na aibu baada ya mume wake kujitokeza wakati wa mkutano wake kupitia Skype akiwa amevalia suruali ya ndani.
Mume wake hakuwa na habari kuwa mke wake alikuwa anajaribu kutatua masuala kadhaa pamoja na wafanyakazi wenzake wakati alikumbana na nyuso geni.