Kando na kuwa mwanahabari shupavu, mtangazaji wa runinga na Citizen TV Lilian Muli amewathibitishia mashabiki wake kuwa anaweza sakata ngoma vilivyo
Kupitia video aliyoipakia kwenye mtandao wa Instagram, Muli akiwa na mpodozi wake binafsi alionyesha umahiri wake katika kunengua kiuno na mashabiki wake bila shaka wamefurahia sana.
” Ni mimi hugundua mambo mengi ikiwa wakati umepita au vipi, tulijivinjari sana mpodoaji wangu @stylistcollins, wewe pia ni rafiki wa dhati, Mungu akubariki,” Alisema Muli.
Muli na mpodoaji wake walikuwa wakisakata ngoma wakati wimbo wa msanii maarufu Otile Brown ukichezwa.