Connect with us

General News

Vijana kupokea mafunzo ya uvuvi katika maji makuu Bahari Hindi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Vijana kupokea mafunzo ya uvuvi katika maji makuu Bahari Hindi – Taifa Leo

TAARIFA ZA WIKI: Vijana kupokea mafunzo ya uvuvi katika maji makuu Bahari Hindi

NA LEONARD ONYANGO

SERIKALI imeanza kutoa mafunzo kwa vijana katika ukanda wa Pwani kuhusu uvuvi kwenye maji makuu ya Bahari ya Hindi katika juhudi za kuongeza mapato ya nchi yanayotokana na samaki wa baharini.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Samaki nchini (KMFRI) James Njiru, anasema mapato ya Kenya yanayotokana na samaki wa baharini yako chini.

“Utafiti uliofanywa umebaini kuwa Kenya ina uwezo wa kupata tani 300,000 za samaki kutoka Bahari ya Hindi kila mwaka. Lakini kwa sasa tunapata tani 26,000 tu,” anasema.

Kwa mfano, Bw Njiru anasema kuwa Kenya hupata tani 1,000 pekee za samaki aina ya ‘tuna’ kutoka Bahari ya Hindi kila mwaka ilhali nchi ya Seychelles inapata tani 200,000. Samaki wa tuna huhama kutoka Seychelles hadi Somalia kupitia Kenya.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending