Hakimu mkuu wa kaunti ya Nyeri aliweza kukamatwa kwa kushirikiana na mauaji ya mume wake aliye uwawa Februari 17,nyumbani kwake Lukenya kaunti ya Machakos.
Hakimu huyo mkuu Pauline Omungala aliweza kuchunguzwa na kuulizwa maswali na polisi wa Athi river jana na kisha kukamatwa na washukiwa wengine.
Mshukiwa huyo mkuu walikuwa na mgogoro wa kinume na mume wake na kisha kuweza kuhama na kumuacha nyumbani mwao Lukenya.
Pauline Omungala na washukiwa wengine watatu wanatarajiwa kuwa mahakani leo ili kujibu mashtaka hayo.

Polisi wataweza kuomba mahakama wakati ili washukiwa hao waweze kuwa rumande wakati uchunguzi unaendelea kufanywa kuhusu mauaji hayo na dhidi ya washukiwa hao.
Waliorumande ni polisi wawili na polisi mmoja aliyestaafu,kukamatwa kwa hakimu huyo pauline kunafuatia baada ya uchunguzi kufanyika katika nyumba ya mwendazake wakili Robert Chesang.
Mkono wa polisi ni mrefu kuliko ule wa mwizi,kwa maana waliweza kujificha wakifikiri kuwa hawataweza kujulikana na kusahau usemi kuwa mbio za nyani uishia jangwani.
Wachunguzi wameweka wazi kuwa mshukiwa mkuu Hakimu Pauline Omungala aliweza kuwalipa wauwaji shillingi 181,000 ili kumuuwa mumewe Robert.
Inaonekana kuwa hakimu huyo aliweza kutambua pesa kuliko maisha ya mume wake ilhali yeye ni hakimu ataweza kuwapa watu aje haki ya kesi yao kama yeye mwenyewe hatambui haki ya mwanadamu kuishi?
“Niliweza kufyatua risasi na tulikuwa tumetumwa na mmoja wa washukiwa ili kumuuwa Robert kwa maana alikuwa ametuarifu kuwa ni jinai,” Alisema polisi mmoja asiyetaka kujulikana.
“Kiini cha mauaji haya baina ya marehemu na mke wake ambaye amekamatwa ilikuwa kwa sababu ya mgogoro wa kifamilia,
“Walikuwa wanapigania mali zao,kisa kilicho wasababisha wawili hao kupelekana mahakani, Pauline aliona kuwa ni haibu kubwa kuenda mbele ya mahakama ilhali yeye ni hakimu,” Alisema polisi anaye chunguza kesi hiyo.
Baada ya wauaji hao kulipwa shillingi 181,000 ili wzweze kutekeleza kitendo hicho hawakusita bali waliweza kufanya kazi yao kisha kutoroka.