DP William Ruto alipokutana na viongozi wa kanisa nyumbani kwake Karen. Picha: William Ruto Source: Facebook
Ruto alinukuu kitabu kitakatifu katika maandiko ya Petro wa kwanza 5:10 ambapo Wakristo wanatakiwa wawe wavumilivu wakati wa mawimbi.
Maandiko ya Petro inawataka wasihofu yote yanayofanyika kwani baadaye anawaahidi kuwa Simba wa Yuda atawaondolea yote
“Na mkisha kuteseka kitambo kidogo, Mungu wa neema yote ambaye amewaita katika utukufu wake wa milele katika Kristo, yeye mwenyewe atawa kamilisheni na kuwathibitisha na kuwatia nguvu,” aliandika DP Ruto kwenye ukurasa wake wa Facebook
DP alisema alikuwa ameshiriki maombi ya asubuhi pamoja na watumishi wa Bwana kutoka kanisa la PCEA na ACK kutoka Mt Kenya wakiongozwa na askofu Charles Muturi. Picha: William Ruto Source: Facebook
DP alisema alikuwa ameshiriki maombi ya asubuhi pamoja na watumishi wa Bwana kutoka kanisa la PCEA na ACK kutoka Mt Kenya wakiongozwa na askofu Charles Muturi.
Haikufahamika mateso aliyokuwa akizungumzia DP Ruto kwenye ujumbe wake lakini kipindi hiki Wakenya wanapitia hali ngumu ya maisha kutokana na janga la covid-19.
Yeye pia amekuwa na kipindi kigumu cha kisiasa huku nyumba yake ikiendelea kuporomoka baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuonekana kuwaangushia bakora wandani wake.