Connect with us

General News

Viongozi waendelea kutuma salamu za pole kwa familia ya John Serut – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Viongozi waendelea kutuma salamu za pole kwa familia ya John Serut – Taifa Leo

TANZIA: Viongozi waendelea kutuma salamu za pole kwa familia ya John Serut

Na WANGU KANURI

VIONGOZI serikalini wamemwomboleza aliyekuwa mbunge wa Mlima Elgon John Serut aliyefariki Jumatano asubuhi katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kansa kwa muda mrefu.

Wakiongozwa na Naibu Rais, viongozi hao wa nyadhifa mbalimbali serikalini wamemtaja mwendazake kama mtu mwadilifu, mwenye bidii na kiongozi shupavu aliyewahudumia vyema watu wa Mlima Elgon.

“Mheshimiwa John Serut alikuwa mwanasiasa imara na jasiri aliyewahudumia watu wa Mlima Elgon kwa utofauti mwingi. Alikuwa mpiganiaji wa usawa na haki. Tunaheshimu urithi ulioacha nyuma,” akaandika Dkt William Ruto.

“Mheshimiwa John Serut alipigania haki na ustawi wa watu wa Mlima Elgon alipohudumu kama mbunge. Alikuwa kiongozi shupavu na imara. Risala zangu za rambirambi zinawaendea wanafamilia wake na watu wa Mlima Elgon. Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi,” akasema Dkt Wycliffe Oparanya.

“Ninamuombea Mama Pamela na familia yake. Mheshimiwa John Serut alikuwa mchapakazi, kiongozi ambaye angetegemewa na aliyeendeleza umoja na maendeleo Bungoma,” akasema Seneta Moses Wetangula.

“Risala zangu za rambirambi ziendee taifa, familia na marafiki wa aliyekuwa mbunge wa Mlima Elgon John Serut. Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi na ailiwaze familia yake katika kipindi hiki kigumu,” akaandika Johnson Muthama.

“Ninasikitika kwa kufariki kwa mheshimiwa John Serut ambaye alikuwa rafiki na mfanyikazi mwenzangu kwenye bunge. Aliwafaa watu wa kaunti ya Bungoma na haswa wakazi wa eneo bunge la Mlima Elgon. Pumzika pema mheshimiwa,” akasema Dkt Boni Khalwale.

Mwendazake alihudumu kama mbunge wa Mlima Elgon mara mbili kati ya mwaka wa 1998 hadi 2007 aliposhindwa na Fred Kapondi.

Hata hivyo, Bw Serut aliwania kiti hicho tena mwaka wa 2013 lakini wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017 akanyanyuliwa tena na Fred Kapondi.

John Serut amefariki akiwa mwenye umri wa miaka 67.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending