Connect with us

General News

Vipusa wa Barcelona wakomoa Chelsea 4-0 na kutwaa taji la UEFA – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na MASHIRIKA

CHELSEA walifungwa mabao manne chini ya dakika 36 za kipindi cha kwanza katika mchuano uliowapa vipusa wa Barcelona fursa ya kutia kapuni taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu huu jijini Gothenburg, Uswidi mnamo Jumapili.

Barcelona walifungua karamu ya mabao katika sekunde ya 33 baada ya Melanie Leupolz kujifunga kisha penalti ya Alexia Putellas katika dakika ya 14 ikafanya mambo kuwa 2-0.

Aitiana Bonmati alifunga bao la tatu la Barcelona katika dakika ya 20 kabla ya Caroline Graham Hansen kuzamisha kabisa chombo cha Chelsea dakika 16 baadaye.

Vipusa wa Barcelona wakomoa Chelsea 4-0 na kutwaa taji la UEFA – Taifa Leo
Barcelona walifungua karamu ya mabao katika sekunde ya 33 baada ya Melanie Leupolz wa Chelsea kujifunga kisha penalti ya Alexia Putellas (pichani) katika dakika ya 14 ikafanya mambo kuwa 2-0. Aitiana Bonmati alifunga bao la tatu la Barcelona katika dakika ya 20 kabla ya Caroline Graham Hansen kuzamisha kabisa chombo cha Chelsea waliopoteza mchezo 4-0. Picha/ AFP

Ushindi huo ndio mnono zaidi kuwahi kusajiliwa na kikosi kwenye fainali ya UEFA ya wanawake.

Yalikuwa matumaini ya kocha Emma Hayes wa Chelsea kuongoza waajiri wake kutwaa mataji mawili msimu huu baada ya kunyanyua ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (WSL). Ilikuwa mara ya kwanza kwa Chelsea kunogesha fainali ya UEFA na ndio wawakilishi wa kwanza wa soka ya Uingereza kushiriki fainali baada ya Arsenal mnamo 2007.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending