– Wabunge sita wa Jubilee watashtakiwa mbele ya kamati ya nidhamu kwa kumkosea heshima kiongozi wa chama
– Baadhi yao ni Sudi na Kuria ambao wanadaiwa kumpaka tope Uhuru Kenyatta kwenye umma
– Ni vita vya pili ndani ya Jubilee baada ya ile iliyowalenga wandani wa DP ndani ya bunge
Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na mwenzake wa Kapseret Oscar Sudi ni baadhi ya viongozi wa chama cha Jubilee ambao wameitwa mbele ya kamati ya nidhamu.
Wengine ni Kimani Ngunjiri wa Bahati, Caleb Kositany wa Soy, Rigathi Gachagua (Mathira) na Alice Wahome wa Kandara.
Mbunge Oscar Sudi. Sudi alisema hatishwi na yeyote ndani ya Jubilee. Ni mmoja wa wale ambao wamepangiwa kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya Jubilee. Picha: Oscar Sudi Source: UGC
Kositany, ambaye pia ni naibu katibu wa chama, alisema yuko tayari kukutana na kamati hiyo lakini akasema mashtaka dhidi yake yafanyike kwenye umma.
“Sina habari kuhusu hatua hiyo lakini naweza kuwaambia wamechelewa, wangekuwa wamefanya hivyo.
“Ombi langu tu ni kuwa mashtaka hayo yaskizwe kwenye umma,” aliongeza naibu huyo wa katibu wa chama Raphael Tuju.