Mkuu wa afya kaunti ya Nakuru Gichuki Kariuki amethibitisha kuwa wafanyakazi 18 kutoka shule ya St. Andrews Turi mjini Molo wamepatikana na virusi vya Corona
Wagonjwa hao 18 walikuwa miongoni mwa visa 23 vilivyoripotiwa kaunti ya Nakuru kati ya Jumatano na Alhamisi wiki hii.
Kufikia sasa Kenya imerekodi zaidi ya visa 8,000 vya maambukizi virusi vya corona siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kufungua mipaka ya Mandera, Nairobi na Mombasa.
Habari zaidi kufuata…
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.