Naibu Chansela huyo alisisitiza kuwa ni lazima wafanyakazi wote wafanyie kazi zao nyumbani nao wenye miaka 58 na zaidi wachukue likizo.
“Tunaendlea kusisitiza kuwa wafanyakazi wafanyie kazi nyumbani.Wale wenye miaka 58 na kuendelea wanaweza kuchukua likizo na kila mmoja ajiweke salama mahali popote alipo,” alisema Kiama.
wafanyakazi watatu wa chuo hicho waliangamizwa na virusi vya corona.Picha:UGC. Source: UGC
Hali hii inakujia wakati vyuo vikuu vinatazamiwa kufungulia mnamo Septemba pamoja na taasisi kama ilivyotangazwa na Wizara ya Elimu.
Aidha, Kiama anadai kuwa wamewasilisha mtazamo wao kuhusu kufunguliwa kwa chuo hicho Septemba ambapo hakutawezana kutokana na kuongezeka maradufu kwa visa vya maambukizi kufikia Novemba.
Kauli ya Kaima inakujia yapata siku chache baada ya Profesa Maurice Kizito Mangoli, mkazi wa Bumula, kumalizwa na na ugonjwa huo wa kupumua akipokea matibabu katika Hospitali ya Nairobi.
Mangoli alikuwa mhadhiri mkuu katika idara ya uhandisi Chuo Kikuu cha Nairobi. Picha:Governor’s Press Service – Bungoma County. Source: Facebook
Hadi kifo chake, Mangoli alikuwa mhadhiri mkuu katika idara ya uhandisi, Chuo Kikuu cha Nairobi.
Gavana wa Bungoma, Wycliffe Wangamati alimuomboleza kama mwalimu aliyetambuliwa duniani, msomi aliyezuru mataifa mengi na mhandisi mwenye maarifa ambaye jina lake lilipachikwa kwenye miradi nyingi ya ujenzi jijini Nairobi.
Idadi ya walioambukizwa virusi vya COVID- 19 sasa imefikia 11,252 baada ya watu wengine 461 kupatikana na virusi hivyo Jumatano Julai 15.
Wizara ya Afya ilitangaza kuwa watu wengine 7 walifariki dunia kutoka na virusi hivyo na kufanya idadi ya vifo kufikia 209.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.