– Manyora amesema mrengo wa handisheki una kibarua kupata mgombea wa kukabiliana na Ruto
– Alisema Ruto i kama kwekwe ambayo humsumbua mkulima kwa uwezo wake kufufuka kila mara
– Mchanganuzi huyo alisema handisheki itapata ushindi tu iwapo mgombea wao atakuwa ni Raila Odinga
Mchanganuzi wa kisiasa Herman Manyora amewataka walio kwenye mrengo wa handisheki kuhakikisha wanacheza kadi zao za kisiasa vizuri la sivyo wapate kichapo 2022.
Mrengo huo wa handisheki unawajumuisha wandani wa Rais Uhuru Kenyatta na wale wa Raila Odinga ambao wanampinga Naibu Rais William Ruto.
Mchanganuzi Herman Manyora asema mrengo wa handisheki una kibarua kigumu kumpata mgombea wao 2022. Picha: Nation Source: Facebook
Kulingana naye, ndiye pekee anaweza kupambana na Ruto kwenye debe la urais ifikapo wakati wa Rais Uhuru Kenyatta kustaafu.
“Hakuna vita ambavyo hajapigana nchini. Na kwa hivyo, ni yeye tu anaweza kumshinda Ruto,” alisema Manyora
“Mrengo wa handisheki lazima ujikune kichwa kuhusu mgombea wao kwa sababu DP Ruto ni kama kwekwe ambayo huishi kumsumbua mkulima kwa uwezo wake kufufuka,” aliongeza
Mchanganuzi huyo alisema licha ya presha na vita vya kisiasa ambavyo DP akubana navyo, angali anawika kisiasa.
“Majina mengi yametajwa kuwania urais: Fred Matiang’i, Gideon Moi, Mudavadi, Kalonzo na Raila. Na hata kama Mt Kenya bado hawajasema lolote, jina la Peter Kenneth limependekezwa na baadhi ya watu ndani ya mrengo wa handisheki,”
Kutoka hii orodha, ni mtu mmoja tu anawezana naye – Raila,” aliongeza Manyora.