Waziri wa Afya Mutahi Kagwe. Picha: MoH Source: UGC
Akitoa takwimu hizo akiwa Nakuru mnamo Alhamisi, Julai 16, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema wagonjwa 512 kati yao walikuwa wakihudumiwa nyumbani kwao huku wengine 58 wakipokea matibabu hospitalini.
Wakati uo huo alitangaza visa vipya 421 vya maambukizi ya coronavirus baada ya sampuli 3, 895 kupimwa.
Idadi ya wagonjwa wa maradhi hayo nchini Kenya sasa imefika 11, 637.
Aidha watu wengine wanane wameaga dunia na kupandisha idadi ya waliopoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo kufika 217.
Alipoulizwa kuhusu maabara ya Lancet ambayo imekuwa na visa vingi vya kutoa matokeo ya vipimo vya kutatanisha Kagwe alisema serikali inafanya uchunguzi ili kuepukana na visa vingine kama hivyo siku za usoni.
“Wizara itachukua hatua. Tumeagiza bodi kuchunguza suala hilo. Hata hivyo, iwapo umekuwa ukisikia maabara ambayo imekuwa ikitoa matokeo ya kukanganya, usiende huko,”
“Kama serikali tuna jukumu la kukagua maabara zote. Baada ya uchunguzi …iwapo itabainika kuwa maabara haifuati maagizo basi tutaifunga,” Kagwe alisema.
Awali TUKO.co.ke iliripoti ilimulikwa baada ya kutoa matokeo ya kukanganya ya walimu 17 wa shule ya St Andrew Turi ambao walipatikana na virusi vya COVID-19.
Siu tatu baadaye walipimwa na kupatikana hawana ugonjwa huo.