– Katibu wa kudumu wa Afya Mercy Mwangangi alitoa takwimu hizo akikagua utayari wa kaunti ya Kwale katika kukabiliana na coronavirus
– Kufikia Jumamosi, Julai 11 idadi ya sampuli zilizopimwa tangu virusi vya corona kutua nchini Machi 2020 ilifika 207, 987
– Jimbo la Kwale liliandikisha wagonjwa 139 ambao kwa sasa wote wamepata nafuu isipokuwa 9 ambao wanahudumiwa wakiwa manyumbani mwao
Katibu katika Wizara ya Afya Dkt Mercy Mwangangi amethibitisha kuwa watu 278 wamepatikana na virusi vya corona na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 9,726.
Akitoa takwimu hizo akiwa kaunti ya Kwale, Mwangangi mnamo Jumamosi, Julai 11 Mwangangi alisema wagonjwa hao walithibitishwa kuambukizwa baada ya sampuli 1,403 kupimwa katika saa 24 zilizopita.
Gavana wa Kwale Salim Mvurya aliwahakikishia wakazi serikali yake imetenga vitanda 340 vya kuwatenga wagonjwa wa homa hiyo kulingana na maagizo ya serikali.
Gavana wa Kwale Salim Mvurya aliwahakikishia wakazi serikali yake imetenga vitanda 340 vya kuwatenga wagonjwa wa homa hiyo kulingana na maagizo ya serikali. Picha: Salim Mvurya. Source: Facebook
Pia alitangaza kwamba kwa siku za usoni hospitali ya Mswambweni itaanza huduma za kuwapima watu.
Wakati huo Mvurya alitoa shukrani zake kwa wizara ya afya kwa kushirikiana nao na kuisadia katika kuthibiti maambukizi.