– Waliilaumu serikali ya Gavana Hassan Joho kwa kuwatenga na kuwabagua wakati wa ugavi wa chakula na bidhaa nyingine muhimu
– Walifunga barabara ya Kibarani na kuapa kutatiza shughuli hadi watakapoletewa chakula
– Hata hivyo polisi waliingilia kati na kuwatawanya baada ya maandamano ahyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari
– Mnamo Aprili, Joho alikuwa akiitisha chakula na misaada nyingine ili kusaidia familia zisizojiweza wakati huu mgumu wa coronavirus
Wakazi wa Kibarani eneo bunge la Changamwe jimbo la Mombasa waliandamana wakitaka chakula cha msaada na maji kutoka kwa serikali ya kaunti wakati janga la corona likizidi kuumiza wananchi.
Wenyeji hao waliokuwa na hasira waliilaumu serikali ya Gavana Hassan Joho kwa kuwatenga na kuwabagua wakati wa ugavi wa chakula na bidhaa nyingine muhimu kwa familia maskini.
Wakazi wa Changamwe waandamana wakilalamikia kunyimwa chakula cha msaada. Picha: Yvonne Mutunga. Source: Original
Waandamanaji hao walianza maandamano yao Ijumaa, Juni 19 na kusababisha msongamano mkubwa wa magari karibu na Kibarani baada yao kuweka vizuizi barabarani.
“Serikali ya kuanri imekuwa ikitupuuza kwa miezi miwili sasa. Sisi tuna familia. Hatuna kazi kutokana na kufungwa kwa biashara zetu na hivyo inakwa vigumu sisi kupata lishe. Kwa nini sasa tunanyimwa chakula?” David Ochieng mmoja wa waandamaji hao aliwaka.
Iliwabidi maafisa wa polisi kuingilia kati ili kuwakabili waandamanaji hao na kufungua barabara kuruhusu magari kupita.
Polisi walilazimika kuingilia kati kukabili hali. Picha: TUKO.co.ke. Source: Original
Licha ya malalamishi hayo, serikali ya kaunti imesalia kimya.
Zoezi la ugavi wa chakula kwa familia zisizojiweza limekubwa na utata huku katika maeneo mengine ikisemekana machifu wanaficha chakula na kuitisha hongo kabla ya kutoa chakula hicho.