Mvua kubwa inayonyesha kaunti ya Kisumu imesababisha madhara makubwa kwa wakazi. Picha: Nancy Okutah. Source: UGC
“Tunaiomba serikali ya kutaifa, ile ya kaunti na wahisani kutusaidia na bidhaa za matumizi nyumbani. Mali yetu yote imeharibiwa na maji. Hatuna chakula. Siku saba sasa hatujaona hatua yoyote ikichukuliwa kutoka kwa serikali,” mmoja wa wakai hao alilalamika.
Mvua hiyo ilianza kunyesha Jumatano, Disemba 25, na kuendelea kwa zaidi ya saa tano huku maji yakifurika katika nyumba za wakazi na kwenye barabara.