Connect with us

General News

Wakazi walilia kaunti imalize uvamizi wa ndovu na viboko – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakazi walilia kaunti imalize uvamizi wa ndovu na viboko – Taifa Leo

Wakazi walilia kaunti imalize uvamizi wa ndovu na viboko

Na WINNIE ATIENO

WAKAZI wa Chakama, Kaunti ya Kilifi wametoa wito kwa serikali kuu kupitia shirika la Huduma za Wanyamapori nchini kutafuta suluhu ya kudumu dhidi ya uvamizi wa ndovu na viboko.

Walisema wanaendelea kukadiria hasara kubwa kila mara ndovu na viboko wanapovamia mashamba yao na kuharibu mimea.

Walisema ukame unaoendelea kukumba baadhi ya maeneo ya kaunti hiyo umechangia uvamizi huo huku wanyama wa pori wakisaka vyakula na maji.

“Ndovu wanatuumiza sana mbona Huduma za Wanyama Pori Nchini isitafute suluhu la kudumu? Niliskia wataalam wa mazingira wakisema hapa ni maeneo ya ndovu, lakini sote twajua wanafaa waishi mbuga zao,” alisema Bw Solomon Mubashiri mkazi.

Bw Mubashiri alisema wakijaribu kufukuza Wanyama hao wanahatarisha maisha yao kwani Wanyama hao ni hatari.Walisema mazao yao yameharibiwa na wanyama hao.

“Nilipanda mahindi ekari tatu n azote ziliharibiwa na viboko,” alisema Bi Chengo Tayari.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending