Connect with us

General News

Wakenya 24 milioni wamejiunga na vyama vya kisiasa, asema Nderitu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakenya 24 milioni wamejiunga na vyama vya kisiasa, asema Nderitu

Wakenya 24 milioni wamejiunga na vyama vya kisiasa, asema Nderitu

Na CHARLES WASONGA

MSAJILI wa vyama vya kisiasa Anne Nderitu anasema jumla ya Wakenya 24.005,714 wamejiandikisha kuwa wanachama wa vyama 82 vya kisiasa vitakavyoshiriki katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Bi Nderitu alitoa tangazo hilo Jumanne, Machi 29, 2022 katika kikao na wanahabari katika afisi yake jijini Nairobi. “Kufikia Jumamosi Machi 26, 2022 muda uliotolewa kwa Wakenya kujiunga na vyama vya kisiasa, jumla ya watu 24,005, 714 walikuwa wamejiunga na vyama vya kisiasa. Kati ya watu hawa, 15, 363, 657 milioni ni wanaume ilhali 8,642, 057 ni wasichana; sawa na asilimia 64 na asilimia 36, mtawalia,” Bi Nderitu.

Bi Nderitu pia alisema kuna jumla ya wawaniaji 17,375 kutoka vyama 68 vya kisiasa ambavyo sajili zao zimekaguliwa kufikia Jumanne, Machi 29, 2022. “Tunataraji kuwa idadi ya wawaniaji itapanda baada ya afisi yangu kukamilisha shughuli inayoendelea ya kukagua na kusafisha sajili za wanachama wa vyama vyote 82,” akaeleza.

Bi Nderitu alisema kuwa shughuli ya kusafisha sajili ya wapiga kura ilianza baada ya Machi 26, 2022 na itakamilika Apili 2, 2022. “Katika muda huo wa siku saba, shughuli ya usajili wa wanachama wapya kidijitali itasimamishwa. Hata hivyo, Wakenya wanaotaka kujiunga na vyama vya kisiasa bado wako huru kufanya hivyo kwa njia ya kawaida katika afisi za vyama hivyo,” akasema.

Bi Nderitu alisema kuwa shughuli ya usafishaji wa sajili za vyama vya kisiasa inajumuisha kuondolewa kwa majina ya watu waliojisajili katika zaidi ya chama kimoja, ikiwa kuna watu ambao umri wao ni chini ya miaka 18 na ikiwa kuna baadhi ya vyama vilivyosajili raia wa kigeni kuwa wanachama.

“Kulingana na sheria ni Mkenya mwenye umri wa miaka 18 pekee ambaye anahitimu kusajiliwa kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa nchini,” akafafanua.