Connect with us

General News

Wakenya waenzi rais aliyeweka maslahi ya taifa mbele ya yake – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakenya waenzi rais aliyeweka maslahi ya taifa mbele ya yake – Taifa Leo

Wakenya waenzi rais aliyeweka maslahi ya taifa mbele ya yake

NA BENSON MATHEKA

WAKENYA wa matabaka mbalimbali Jumatatu walijitokeza kwa wingi katika Majengo ya Bunge kutoa heshima zao za mwisho kwa rais wa tatu, marehemu Emilio Mwai Kibaki.

Kibaki alifariki Ijumaa akitibiwa katika Nairobi Hospital akiwa na umri wa miaka 90.

Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa Katoliki Kadinali John Njue aliongoza sherehe fupi ya kidini kabla ya mwili kuanza kutazamwa na umma.

“Nilifurahia utawala wa Kibaki kwa kuwa uchumi ulikuwa bora na ndio sababu nimefika kumpa heshima zangu za mwisho,” akasema Bw Joseph Ogodo, mkazi wa mtaa wa Mathare jijini Nairobi.

Mwalimu Jimmy Kimani alisema kuwa alifika kutoa heshima za mwisho kwa Kibaki kwa kuwa aliboresha masomo nchini: “Nimefika hapa kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi aliyejali masomo ya watoto wa nchi hii.”

Mwili wa marehemu atakayezikwa Jumamosi nyumbani kwake Othaya, Kaunti ya Nyeri utalazwa katika majengo ya Bunge hadi Jumatano ili raia waweze kutoa heshima za mwisho.

Mnamo Alhamisi, utapelekwa Ikulu ya Nairobi kabla ya ibada ya wafu ya kitaifa kufanywa Ijumaa katika uwanja wa michezo wa Nyayo ambako viongozi wa mataifa mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending