Picha ya baada ya mkutano aliyopigwa wakili matata ambaye ni raia wa Kenya Miguna Miguna akiwa na rafiki yake imewafanya baadhi ya marafiki zake mitandaoni kuhofia hali yake na kuitaka serikali kumruhusu arejee nchini.
Miguna Miguna akiwa na rafiki yake Jackson Igbinosun katika kituo cha Black Gold Think Tank. Picha: Miguna Miguna Source: Facebook
Kwenye picha hiyo, Miguna alisimama na rafiki yake Jackson Igbinosun katika kituo cha Black Gold Think Tank.
Lakini kilichowashangaza mashabiki wake ni mwonekano wake, alikuwa na kidevu ambacho siku nyingi hakijakutana na mkasi ama wembe na mwili wake ulikuwa umepungua unene.
Kulingana na wengi, alionekana mzee, aliyechoka sana, na asiye na ukakamavu, na baadhi walitania anakuwa mzee kabla ya kuwakomboa kutoka kwenye meno ya “udikteta”.