[ad_1]
Wakili ashtakiwa kwa kutumia lifti ya Rais katika KICC
Na RICHARD MUNGUTI
WAKILI ameshtakiwa kwa kuwatusi maafisa wawili wa polisi waliomzuia kutumia njia ambayo hutumiwa na Rais Uhuru Kenyatta ndani ya jumba la KICC, Nairobi.
Kincy Nangami Wafula, 29, alikanusha mashtaka mawili ya kutusi afisa msimamizi wa kituo cha polisi cha KICC na Sajini Susan Misoi. Bi Wafula anadaiwa kutenda uhalifu huo alipokutwa akitafuta mahala pa kujisaidia katika jumba la KICC.
Wakili huyo alikanusha shtaka la kuwatukana OCS, Catherine Otieno na Sajini Susan Misoi. Bi Wafula alikumbana na maafisa hao wa polisi alipokuwa akitafuta mahali pa kujisaidia.
Alielekezwa na mfagiaji eneo alilokutwa na maafisa hao wa polisi.
Wakati wa mahojiano alichokuwa akifanya eneo hilo lisilokubaliwa watu kutembelea, mshtakiwa aliwaeleza hakujua kwa vile yeye ni mgeni. Ni wakati huo hasira ilimpanda ndipo akawatukana polisi matusi tusiyoweza kuyachapisha.
Alikabiliwa na shtaka la kutumia lugha chafu kwa polisi na kukataa kutiwa nguvuni. Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh20,000.
Next article
KPA kutumia Sh2m kusaidia wahanga wa njaa
[ad_2]
Source link