Connect with us

General News

Wakongwe walalamikia foleni ndefu wakati wa malipo ya Inua Jamii – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakongwe walalamikia foleni ndefu wakati wa malipo ya Inua Jamii – Taifa Leo

Wakongwe walalamikia foleni ndefu wakati wa malipo ya Inua Jamii

KENYA NEWS AGENCY na CHARLES WASONGA

WAKONGWE katika eneo la Igembe, kaunti ya Meru wamelalamikia mateso wanayopitia wapolazimika kupiga foleni ndefu kuchukua ruzuku zao chini ya mpango wa Inua Jamii.

Wazee hao wamekuwa wakifika kwa wingi katika afisi za idara ya huduma za kijamii mjini Maua kupokea pesa zao.

Jumatatu, walimkabili Afisa wa Idara ya Ustawi wa Kijamii Francis Mwangi wakimtaka aelezee ni kwa nini wanalazimika kukaa katika foleni kwa muda mrefu.

Zaidi ya wakongwe 1000 kutoka familia mbali waliambia KNA kwamba licha ya Bw Mwangi kuwahakikishia mara kadha kwamba malalamishi yao yatashughulikiwa, hajapata afueni.

Wengi wao, ambao wanazongwa na uzee na matatizo ya kiafya, walilalamika kuwa wanaathiriwa na hali mbaya ya anga wanapopiga foleni nje ya afisi za idara hiyo

Wazee hao wenye umri wa miaka 70 kwenda juu, wamekuwa wakipitia masaibu tangu Novemba mwaka jana.

Ni wakati huo ambapo serikali ipoagiza kwamba wazee hao wasajiliwe upya na wafungue akaunti katika benki ili pesa zao ziwe zikipitishwa kwa akaunti hizo.

Hii ni baada ya muda wa utekelezaji wa mkataba wa awali kati ya serikali na taasisi za kifedha kuisha.

Wakati huo, benki sita zilikuwa zimepewa zabuni ya kuwa vituo vya utoaji wa pesa hizo kwa wakongwe hao.

Walitoa wito kwa serikali kuu kugatua vituo vya utoaji pesa hizo hadi ngazi ya vijijini ili kuwakinga na usumbufu wa kusafiri hadi mjini Mau.

“Sina nguvu ya kusafiri kwa mwendo wa kilomita 10 kutoka nyumbani kuja hapa kupokea hizi pesa. Hii ni kwa sababu nimekuwa nikiugua kwa miaka 20 iliyopita. Huduma hii iletwe kule kwetu vijijini au katika afisi ya chifu,” mzee mmoja akaambia KNA.

Wakati huo huo, wazee kutoka sehemu mbalimbali nchini wamelalamikia mwenendo wa maajenti wa benki mbali mbali kukata pesa zao.

Katika kaunti ya Homa Bay baadhi ya wazee wamalalama kwamba maajenti hao wanakata kati ya Sh500 na Sh1,000 wanazodai kama “ada ya huduma”.

Visa sawa na hivyo, vimeripotiwa katika maeneo bunge ya Bahari na Njoro katika kaunti ya Nakuru.

Serikali kupitia Idara ya Huduma kwa Wakongwe, wiki jana ilianza kusambaza Sh8,000 kwa wakongwe. Pesa hizo ni malimbizi ya miezi minne kuanzia Julai ya Novemba, 2021.

Chini ya mpango wa Inua Jamii serikali hutoa ruzuku ya Sh2,000 kwa makundi wenye mahitaji maalum kama vile wazee, mayatima na watu wanaoishi na ulemavu.

Zaidi ya watu milioni moja wamesajili kwa mpango huu.