Connect with us

General News

Wakulima wa kahawa wavuna mamilioni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakulima wa kahawa wavuna mamilioni – Taifa Leo

Wakulima wa kahawa wavuna mamilioni

NA VITALIS KIMUTAI

WAKUZAJI kahawa katika kaunti za Kericho, Bomet na Nandi wamepokea Sh105.1 milioni kutokana na mauzo ya kahawa nchini Korea Kusini.

Wakulima hao wapatao 9, 852 waliuza jumla ya tani 134.4 milioni za kahawa nchini humo chini ya mwavuli wa Chama cha Ushirika cha Wilaya ya Kipkelion.

Mauzo hayo yanafuatia mageuzi mapya yaliyofanywa na serikali kulainisha sekta ya kahawa nchini. Mnamo Februari 10 mwaka huu,

chama hicho kilisafirisha kahawa hiyo nchini humo kupitia kampuni ya Good Beans. Hatua hiyo ilifuatia mwafaka uliofikiwa Julai mwaka ja – na wakati wa Maonyesho ya Kahawa ya Seoul, yaliyofanyika nchini humo.

“Kutokana na mwelekeo huo mpya, wakulima wamelipwa wastani wa Sh116 kwa kilo moja ikilinganishwa na Sh76 hapa nchini. Hiyo ni tofauti ya Sh40,” akasema Gavana Paul Chepkwony wa Kaunti ya Kericho.

Prof Chepkwony aliisifu serikali kutokana na mageuzi hayo, ambapo sasa wadau katika sekta hiyo wako huru kutafuta masoko ya zao

hilo ng’ambo ili kuhakikisha wakulima wanapata bei bora zaidi. “Kutokana na mageuzi hayo, wakulima sasa watapata faida kubwa zaidi kutokana na mauzo ya mazao yao kwa kuwa mageuzi hayo yaliwaondoa mawakala walaghai ambao walikuwa wakiwapunja kwa muda mrefu,” akasema gavana huyo.

Alisema hayo alipokuwa akitoa hundi za malipo kwa wakulima katika eneobunge la Kipkelion Magharibi.Jumla ya vyama 67 vya ushirika katika eneo hilo vimeungana na kubuni Chama cha Ushirika cha Wilaya ya Kipkelion, ambacho huzalisha

na kuuza kahawa yao. Chama hicho pia kimepata nafasi nyingine kuuza tani milioni 40 za kahawa katika taifa lilo hilo. Kulingana na balozi wa Kenya nchini humo, Bi Mwende Mwinzi, ubalozi huo umekuwa ukiweka mikakati ya kuivumisha Kenya kibiashara katika nchi hiyo.

“Kuuzwa kwa kahawa hiyo ni jambo la kihistoria. Ni jambo la kipekee pia ikizingatiwa ilisafirishwa katika Bandari ya Mombasa kwa Reli ya Kisasa (SGR). Hii ni mara ya kwanza kwa kahawa kutoka Kenya kuuzwa moja kwa moja nchini humu.”