Connect with us

General News

Wakulima wahimizwa wasivune makadamia kabla hayajakomaa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wakulima wahimizwa wasivune makadamia kabla hayajakomaa – Taifa Leo

Wakulima wahimizwa wasivune makadamia kabla hayajakomaa

Na LEONARD ONYANGO

WAKULIMA wametakiwa wasivune mazao yao ya makadamia kabla ya hayajakomaa.

Madalali wamekuwa wakinunua mazao hayo ambayo hayajakomaa kwa Sh50 kwa kila kilo na kisha kuyahifadhi wakingojea kuyauza mwezi Machi wakilenga kujipatia faida kubwa.

Wakati wa mavuno kati ya Machi na Julai, kilo moja ya makadamia huuzwa kati ya Sh170 na Sh200.

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Makadamia katika Kaunti ya Meru, Joshua Muriira, anasema kuwa wakulima wamekuwa wakivuna mazao ambayo hayajakomaa ili kupata fedha za kulipia watoto wao karo.

Wataalamu wanahofia kuwa hatua ya wakulima kuvuna zao hilo kabla ya kukomaa huenda ikasababisha makadamia ya Kenya kupigwa marufuku katika soko la kimataifa.