[ad_1]
MAPISHI KIKWETU: Wali na nyama
NA MARGARET MAINA
[email protected]
Muda wa kuandaa: Dakika 15
Muda wa mapishi: Dakika 30
Walaji: 4
Vinavyohitajika kwa wali
- mchele kilo ½
- tui la nazi kikombe 1
- maji mara mbili ya kiasi cha mchele
- chumvi
Maelekezo
Osha mchele.
Weka mchele jikoni na ongeza chumvi. Acha mchele hadi uanze kuchemka.
Ukishaanza kuchemka, ongeza tui la nazi. Usikoroge.
Acha mchanganyiko uive taratibu kwa dakika 10.
Punguza moto na uache wali uive hadi maji yakauke.
Epua.
Vinavyohitajika kwa nyama
nyama kilo 1
vitunguu maji 2
vitunguu saumu 2
tangawizi 1
nyanya 4
mafuta ya kupikia
chumvi kijiko 1
pilipili mboga 1
Maelekezo
Menya vitunguu na pilipili mboga na ukate viwe vipande vyembamba sana.
Menya nyanya na tangawizi kisha ukatekate.
Twanga vitunguu saumu kisha bandika sufuria ya kupikia jikoni.
Weka nyama na anza kukoroga ishikilie kwenye sufuria na ikauke.
Weka kitunguu maji huku ukiendelea kukoroga kwa muda wa dakika 10.
Ongeza kitunguu saumu na tangawiizi huku ukikoroga.
Weka mafuta ya kupikia kisha weka pilipili mboga. Ongeza chumvi kidogo. Endelea kukoroga.
Weka nyanya, koroga na funika sufuria kisha uache kwa dakika 10.
Pakua na ufurahie.
Next article
PDP: Obado asalia mpweke wawaniaji wakikwepa chama
[ad_2]
Source link