WALIMU kote nchini wameingiwa na tumbojoto kuhusu uhamisho ambao Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) inatekeleza kabla ya muhula ujao.
Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC, Nancy Macharia ameeleza kuwa shughuli hiyo itawasawazisha walimu kulingana na idadi ya wanafunzi katika shule kabla ya mwaka mpya wa masomo kuanza.