Connect with us

General News

Walimu wanawasaliti wazazi kupendekeza karo iongezwe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Walimu wanawasaliti wazazi kupendekeza karo iongezwe – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Walimu wanawasaliti wazazi kupendekeza karo iongezwe

NA WANDERI KAMAU

DUNIA inapitia hali ngumu sana ya kiuchumi. Kila mmoja analia kutokana na ugumu wa hali ya maisha.

Cha kusikitisha ni kuwa, Benki Kuu ya Dunia, Shirika la Fedha Duniani (IMF) kati ya taasisi nyingine za kifedha, zimetabiri kuwa hali hiyo itazidi kudorora, hasa kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Kuutia msumari kwenye kidonda, nchi nyingi bado hazijajitoa kwenye makovu ya athari za kiuchumi za janga la virusi vya Corona.

Katika hali hiyo, ni wazi kuwa mamilioni ya Wakenya, sawa na watu wengine duniani, wanapitia katika mojawapo ya hali ngumu zaidi za kimaisha kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Wadadisi wa masuala ya kiuchumi na kisiasa wanasema, hali ya sasa ilishuhudiwa tu baada ya kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, vilivyodumu kati ya 1939 na 1945.

Chini ya hali hiyo, juhudi tunazopaswa kuona kutoka kwa wasimamizi na waendeshaji wa sekta mbalimbali nchini, ni mikakati ya kuwasaidia Wakenya kukabili ugumu huo. Hata hivyo, inasikitisha kuwa, serikali inaonekana kutomjali Mkenya, hasa baada ya walimu wakuu wa shule za upili kupendekeza kuongeza karo za shule kwa hadi Sh16,000.

Walimu hao walitoa pendekezo hilo kwenye Kongamano lao la Kila Mwaka, linalokamilika leo jijini Mombasa.

Ikizingatiwa kuwa baadhi ya walimu hao ni wazazi, kinachoibua maswali ni ikiwa wao hawahisi ugumu na changamoto nyingi ambazo wazazi wengi wanapitia kuwalipia karo wanao kwa sasa. Tangu kuibuka kwa janga la Corona mnamo Machi 2020, sekta ya elimu ni miongoni mwa zile zilizoathirika pakubwa.

Wanafunzi walilazimika kukaa nyumbani kwa karibu miezi kumi, hadi pale maambukizi ya virusi hivyo yalipopungua.

Baada ya wanafunzi kurudi shuleni, Wizara ya Elimu ilibuni ratiba kali, ili kuwawezesha wanafunzi kurejelea masomo yao kama ilivyokuwa hapo awali.

Ni ratiba ambayo inawalazimu wazazi kulipa kiasi kikubwa cha karo kwa wanafunzi wao baada ya muda mfupi mno. Kinyume na ilivyokuwa hapo awali, wazazi hawajakuwa wakipata muda wa kutosha wala nafasi ya kupumzika kutafuta karo.

Bila shaka, ni wazi kuwa ratiba hiyo imewahangaisha sana wazazi kifedha. Rai za baadhi yao kwa wasimamizi wa shule angaa kuwaongeza muda kutafuta karo zimekuwa zikifutiliwa mbali.

Wito mkuu kwa serikali na wasimamizi wakuu wa elimu nchini, ni kutowaongeza mzigo wazazi kutokana na changamoto wanazopitia. Huu ndio wakati mwafaka kusikiza kilio chao.

[email protected]