Connect with us

General News

Wanafunzi wa shule za mchana wang’aa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanafunzi wa shule za mchana wang’aa – Taifa Leo

Wanafunzi wa shule za mchana wang’aa

NA MARY WANGARI

WANAFUNZI wa shule za viwango vya kaunti ndogo waling’aa kwenye Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) 2021 huku jumla ya 128 miongoni mwao wakijizolea alama kuanzia A- kwenda juu.

Anthony Njuguna Muhoro kutoka Shule ya Sekondari ya Kiamaina iliyopo Eneo la Bonde la Ufa, ndiye mwanafunzi nyota katika shule za kiwango cha kaunti ndogo.

Anafuatiwa na Eric Owino (Shule ya Sekondari ya Akoko), Clinton Karwitha (Shule ya Sekondari ya Mseto ya Angaine) Dillan Alukoti (Shule ya Sekondari ya Matunda S.A.) Frank Ndiangui (Shule ya Sekondari ya St James Kiaritha) kutoka Kaunti za Nyanza, Mashariki, Magharibi na Eneo la Kati Mtawalia.

Denis M’Kirima (Shule ya Sekondari ya Charles Lwanga katika eneo la Pwani na Ronald Kipkoech kutoka Shule ya Sekondari ya Kiplabotwa, Kaskazini Mashariki, ni miongoni mwa wanafunzi wa shule za viwango vya kaunti ndogo waliotia fora kwenye KCSE 2021.

Akitangaza matokeo ya KCSE 2021 Jumamosi, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha alisema kwamba wanafunzi zaidi ya 17,000 kutoka shule za mchana wamepata kuanzia alama C+ kwenda juu.

Hii ina maana kuwa idadi kubwa ya wanafunzi kutoka shule za mchana wamefuzu kujiunga na vyuo vikuu vya umma nchini baada ya kupata alama kuanzia C+ ambayo kwa kawaida inahitajika ili kuweza kujiunga na vyuo vikuu vya umma nchini.

“Katika mtihani wa KCSE 2021, wanafunzi katika shule za sekondari za viwango vya kaunti ndogo ambazo aghalabu ni shule za mchana, waliandikisha matokeo ya kufana. Jumla ya wanafunzi 17,327 walipata alama ya C+ kwenda juu, huku 128 miongoni mwao wakipata alama A- na kwenda juu,” alisema Waziri Magoha.

“Hii inaonyesha kuwa watoto wanaweza kutia fora katika shule za mchana za viwango vya kaunti ndogo,”alisema.

Shule kumi bora za viwango vya kaunti ndogo zinaongozwa na Shule ya Sekondari ya Nyakeore (Kaunti ya Nyanza) Shule ya Sekondari ya Kebulonik (Bonde la Ufa) Shule ya Sekondari ya Mseto ya Banisa (Kaskazini Mashariki) Shule ya Sekondari ya Mseto ya Manyatta (Mashariki) na Shule ya Sekondari ya Mseto ya Shibanga.

Shule ya Sekondari ya Heni (Eneo la Kati), Shule ya Sekondari ya Mary Happy Day  (Nairobi), Shule ya Sekondari ya Alfasy Girls (Pwani).

Katika mtihani wa 2020 ni kaunti 15 ambazo ziliandisha idadi ya juu ya watahiniwa wasichana kuliko watahiniwa wavulana.

Kaunti 18 ambazo zilikuwa na idadi ya juu ya watahiniwa wasichana katika KCSE ya 2021 zilikuwa ni;

Taita Taveta, Nyandarua, Nyeri, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Machakos, Kitui, Meru, Elgeyo Marakwet, 29 Busia, Kakamega, Vihiga, Tharaka Nithi, Nairobi, Uasin Gishu, Laikipia na Kisumu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending