– Kumekuwa na wasiwasi kwenye nyanja ya uanahabari baada vituo kadhaa kuwafuta kazi watangazaji wake
– Sasa watangazaji wameanza kuwekeza kwenye biashara mbadala kuepuka pigo la mapato wanapofutwa kazi
– Ben Kitili alifichua kuwa kwa sasa anajihusisha na ufugaji wa mbuzi
Huku ulingo wa uanahabari ukionekana kuyumbayumba ambapo wengi wanazidi kupoteza kazi kila uchao, ni wazi sasa waliobaki wameamua kutafuta njia mbadala za kujikimu.
Wengi wa wanahabari sasa wameanza kuwekeza katika biashara zao kibinafsi ili kuepuka pigo kifedha wanapoangukiwa na shoka la mwajiri.