Mungai Gathogo aliyepewa tenda ya kuwasilisha vitanda 500 kwa serikali ni mwanasiasa wa Kiambu. Picha: PDU Source: UGC
Wawili hao wanaundia vitanda hivyo katika eneo la Githunguri kaunti ya Kiambu ambapo Rais alituma kikosi chake kukutana na wao.
Hata hivyo, uamuzi wa Rais ulizua hisia kali mitandaoni kwani serikali haikua imetoa uamuzi wa kununua vitanda kama hivyo kutoka kwa fundi mwingine kwa jina Meshack Otieno.
Wanamtandao walidai kuwa Otieno ndiye alikuwa wa kwanza kuunda vitanda namna hiyo na Rais kuwapa kazi Muhinja na Gathogo ilikuwa ni mapendeleo.
Mwangi Gathogo aliwania useneta katika kaunti ya Kiambu 2017. Picha: PDU Source: Facebook
Kwenye mahojiano na TUKO.co.ke, Gathogo alisema ni mwanasiasa na aliwania kiti cha useneta katika kaunti ya Kiambu.
“Ni kweli niligombea kiti cha useneta 2017 lakini sikufika kwenye debe. Kama kijana, nilikuwa najaribu lakini mambo hayakuenda vizuri na nikajitoa kwenye mchujo,” alisema.
Alisema awali alikuwa akiuza vieuzi na kisha akaamua kuingilia biashara ya kuuza vitanda hivyo baada ya kugundua vinahitajika sana.
Mabango ya Gathogo Mwangi kwenye kampeni za 2017. Picha: UGC Source: UGC
Alisema aligundua kuhusu fundi mwenzake, Meshak, baada ya kuchapisha picha za vitanda zake kwenye mtandao.
“Niligundua kumhusu baada ya siku tatu nilipochapisha picha kwenye ukurasa wangu wa Facebook, ndipo video yake ikajiri,” alisema.
Alisema siasa zake hata hivyo hazikuchangia kwa vyovyote katika kupata tenda ya serikali ambayo kwa sasa inazungumziwa na wengi.
“Siasa zangu hazina lolote kuhusiana na tenda hiyo. Mimi sikumuita mtu yeyote hata kama mimi ni mwanasiasa na mfuasi wa Naibu Rais William Ruto,mimi sikujua hata mkuu wa PDU,” alisema.
Mkuu wa kitengo cha Rais cha PDU Andrew Wakahiu alizuru eneo hilo na kusema serikali itasaidia Gathogo kupanua biashara yake ili waweze kuwasilisha vitanda 500 kwa mwezi mmoja ujao.