Connect with us

General News

Wanasiasa wahimizwa wasitishe kampeni kwa heshima ya Kibaki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wanasiasa wahimizwa wasitishe kampeni kwa heshima ya Kibaki – Taifa Leo

Wanasiasa wahimizwa wasitishe kampeni kwa heshima ya Kibaki

NA MWANGI MUIRURI

WANASIASA katika eneo la Mlima Kenya wametakiwa kutocheza muziki na kupiga kelele kwenye kampeni zao kama ishara ya kutoa heshima kwa rais wa tatu wa Kenya, Mwai Kibaki aliyefariki dunia Ijumaa.

Wanasiasa katika eneo la Mlima Kenya wamekuwa wakizunguka vijijini huku wamebeba maspika makubwa juu ya magari yao wakijinadi kwa wakazi.

Kibaki aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 90 na shughuli ya kutazama mwili wake katika majengo ya Bunge iling’oa nanga Jumatatu na itakamilika kesho Jumatano.

Gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria alisema Jumatatu kuwa tayari amesitisha kampeni zake za urais katika kipindi hiki cha maombolezo kitakachoisha baada ya mazishi ya Kibaki eneo la Othaya, Kaunti ya Nyeri, Jumamosi.

Bw Wa Iria alimtaja Kibaki kama “kiongozi aliyekuwa mzalendo na shujaa ambaye mchango wake kwa taifa utasalia katika vitabu vya kumbukumbu”.

Gavana wa Nyandarua, Francis Kimemia alisema mazingira yenye utulivu bila kelele za kisiasa ni muhimu wakati wa kuomboleza kiongozi aliyekwamua nchi kutoka kwa masaibu ya kiuchumi.

Mwenyekiti wa vuguvugu la madiwani kutoka eneo la Mlima Kenya, Charles Mwangi, aliwataka wanasiasa kukomesha siasa wakati huu wa majonzi.

“Muda wa kuanza rasmi kampeni haujafika hivyo wanasiasa hawana budi kujiepusha na kampeni za mapema; watoe fursa kwa Wakenya kuomboleza kiongozi wao,” akasema Bw Mwangi.

Seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata ambaye yuko ziarani nchini Amerika alisema kuwa Wakenya wanafaa kutumia kipindi hiki cha maombolezi kutafakari mema yaliyofanywa na Kibaki.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending