– Viongozi hao walikutana nyumbani kwa mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri na kujadili siasa za 2022
– Ngunjiri na wenzake kutoka jamii ya Mlima Kenya waliahidi wenzao kutoka Baringo kuwa licha ya presha, wangali nyuma ya DP
– Wabunge wa Mlima Kenya ambao humuunga mkono DP wamekuwa wakipigwa kisiasa na mrengo wa Rais Uhuru
Viongozi wanaoegemea mrengo wa kisiasa wa Naibu Rais William Ruto Jumamosi, Julai 18 walifanya mkutano Nakuru kujadili mwelekeo wao kwenye safari ya 2022.
Seneta wa Nakuru Susan Kihika, wabunge Moses Kuria, Liza Chelule, Caleb Kositany pamoja na viongozi wengine walikutana nyumbani kwa Kimani Ngunjiri wa Bahati.
Wandani wa DP Ruto walifanya mkutano pamoja na wenzao kutoka Baringo Jumamosi Julai 18. Picha: Susan Kihika Source: Facebook
Mdokezi aliarifu TUKO.co.ke kuwa mkutano huo uliandaliwa na Ngunjiri na ulikuwa wa kuhakikishia viongozi hao kutoka Baringo kuwa bado wako nyuma ya DP Ruto.
Viongozi hao walisema kama Rais Uhuru Kenyatta alivyoahidi 2013 kuwa jamii ya Mlima Kenya itamuunga mkono Ruto, wao wangali wameshikilia msimamo huo.
Ngunjiri alisema umoja kati ya jamii za bonde la ufa ulioletwa na ushirikiano kisiasa kati ya Ruto na Uhuru unafaa kulindwa kwa kumuunga mkono DP 2022.
Licha ya kusema wanapokea presha kwa kumuunga DP, Mbunge Kimani Ngunjiri alisema wako nyuma yake mpaka mwisho. Picha: Ngunjiri Source: Facebook
Kihika, Ngunjiri na Kuria ni baadhi ya wafuasi sugu wa DP kutoka eneo la Mlima Kenya ambapo kampeni kali inaendelea ya kuwataka viongozi kukoma kumuunga mkono Ruto.
Wote ambao wamekuwa wakimpigia debe Ruto wameangukiwa na bakora ya Rais Uhuru Kenyatta kwa kutimuliwa kutoka nyadhifa walizokuwa wakishikilia chamani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.