[ad_1]
Wanne wazuiliwa siku saba kwa kutumia kileo kuwapumbaza abiria
NA RICHARD MUNGUTI
WANAUME wanne watazuiliwa kwa siku saba kwa kuhojiwa kubaini ikiwa walihusika katika kuwapumbaza wasafiri kutoka Kisumu hadi Nairobi.
Washukiwa hao Stephen Odero, Benson Hamisi, Harrison Nyamu na Joshua Orengo walikamatwa katika kituo cha polisi cha Kabete baada ya dereva wa basi hilo kulipeleka kituoni uchunguzi ufanywe.
Dereva wa basi hilo aligudua abiria walikuwa wameleweshwa na kupambazwa na kile alichodai ni kupuliziwa kileo.
Walikuwa wamelala fofofo kutoka Kisumu.
Abiria hao walilalamika wamepoteza pesa , simu na vifaa vya thamani kama vile laputopu.
Washukiwa hao wanne walikutwa na bidhaa hizo.
Polisi waliwatia nguvuni washukiwa hao wanne walipokutwa na baadhi ya bidhaa zilizopotea kutoka abiria hao
Konstebo James Kariuki aliomba muda akamilishe uchunguzi pamoja na kuandikisha taarifa za mashahidi.
“Baada ya dereva kuelezewa abiria wameleweshwa na kupambazwa alipeleka basi katika kituo cha polisi cha Kabete,” hakimu mkazi Renee Kitangwa alifahamishwa na Konstebo Kariuki.
“Baada ya kusikiliza ushahidi wa Kariuki nimeridhika anahitaji muda kukamilisha uchunguzi. Washukiwa watazuiliwa kwa siku saba,” Bw Kitangwa aliagiza.
Washtakiwa watazuiliwa kwa siku saba kuhojiwa katika kituo cha Kabete na wakati huo huo abiria kuandikisha taarifa za ushahidi.
Next article
Nottingham Forest warejea EPL baada ya miaka 23
[ad_2]
Source link