Connect with us

General News

Wapwani washauriwa wakome kubagua wanaougua Ukimwi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wapwani washauriwa wakome kubagua wanaougua Ukimwi – Taifa Leo

Wapwani washauriwa wakome kubagua wanaougua Ukimwi

NA MAUREEN ONGALA

WATAALAMU wa kiafya wametaka jamii za eneo la Pwani kukomesha unyanyapaa dhidi ya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi eneo hilo.

Afisa anayehusika na masuala ya kudhibiti ueneaji wa virusi vya Ukimwi katika Kaunti ya Kilifi, Bw Joseph Kapombe, alisema bado kuna wananchi ambao hukataa kushirikiana ama kujumuika na wale walioambukizwa virusi hivyo nyumbani au katika sehemu za umma.

Akizungumza katika warsha iliyoandaliwa Kilifi, Bw Kapombe alisesema kuwa hatua hiyo imeendelea kuwaathiri wagonjwa hao kisaikolojia na kufanya wengine wasikubali hali yao, na hivyo kukosa kufuata mashauri ya kujilinda kiafya.

Warsha hiyo ilikuwa imeandaliwa wiki iliyopita ili kuhamasisha viongozi wa kidini na jamii kuhusu Ukimwi katika eneo la Malindi na Magarini.

Bw Kapombe alisema idadi ya maambukizi miongoni mwa vijana inaongezeka zaidi katika jamii kutokana na baadhi yao kutofuata ushauri wa afya, kuhusiana na masuala ya jinsi wanavyoweza kujikinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Aidha, amelalamikia hatua ya vijana walioathirika pia kukumbwa na changamoto nyingi hasa wale walioko shuleni, ikiwemo suala la walimu pamoja na wanafunzi wengine kuwatenga.

“Wanafunzi wakiwa shuleni wanabaguliwa na kuendelea kupata unyanyapaa kutoka kwa walimu, wafanyikazi na hata wanafunzi wenzao,” akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending