– Waruguru amewataka wakazi wa Laikipia kuunga mkono utendakazi wa Rais Uhuru Kenyatta ili wanufaike kutokana na miradi ya maendeleo
– Kulingana na mwanasiasa huyo, Uhuru atazindua miradi kadhaa hivi karibuni akishirikiana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga
– Mbunge huyo alidai Tangatanga haina mwelekeo wa kimaendeleo kwa wananchi
– Waruguru kwa wakati mmoja aliwahi kuwa mwanadani wa karibu wa Naibu Rais William Ruto na mkosoaji mkuu wa uongozi wa Uhuru
Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Laikipia Cate Waruguru amesema hatakufa moyo kuwahamasisha wakazi wa kaunti hiyo kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta katika utendakazi wake
Waruguru alisema wakazi wa eneo bunge lake watanufaika zaidi kutokana na miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa na Rais kwa sasa.
” Miradi ya maendeleo haipatikani katika kikundi cha Tangatanga ila serikalini, hebu na tumuunge mkono Rais katika kutekeleza wajibu wake,” Alisema Waruguru.
Waruguru pia aliwahakikishia wakazi kuwa Rais Uhuru Kenyatta anapanga kuzindua miradi kadhaa atakapozuru eneo hilo akiwa na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.
Itakumbukwa kuwa Waruguru alikuwa mwandani wa karibu wa naibu Rais ila alimgeuka hivi majuzi na kujiunga na kikundi cha Kieleweke ambacho kinaongozwa na viongozi wanaomuunga mkono Rais.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.