Connect with us

General News

Watimkaji Chepchirchir, Kiplagat waendea Sh1.1m New York Mini 10K – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Watimkaji Chepchirchir, Kiplagat waendea Sh1.1m New York Mini 10K – Taifa Leo

Watimkaji Chepchirchir, Kiplagat waendea Sh1.1m New York Mini 10K

Na GEOFFREY ANENE

MALKIA wa Boston Marathon Peres Jepchirchir amethibitisha kushiriki mbio za New York Mini 10K mnamo Juni 11.

Mkenya huyo, ambaye alinyakua mataji ya mbio za kilomita 42 ya Olimpiki na New York mwaka 2021, anawania taji dhidi ya Waamerika Emily Sisson, Molly Seidel, mzawa wa Kenya Aliphine Tuliamuk na Rachel Smith.

Pia, kuna mshindi wa New York Half-Marathon Muethiopia Senbere Teferi, ambaye anashikilia rekodi ya dunia mbioza kilomita tano, na bingwa mara mbili wa New York Mini 10K Sara Hall kutoka Amerika pia yupo katika orodha ya watimkaji.

Bingwa wa zamani wa marathon za New York, London na Boston Edna Kiplagat kutoka Kenya anarejea New York Mini 10K aliyoshinda mwaka 2012.

Viola Cheptoo, ambaye alikamilisha New York Marathon na New York Mini 10K katika nafasi ya pili mwaka jana, bingwa wa mbio za mita 10,000 za vyuo vya Amerika, Canada na Puerto Rico (NCAA) Sharon Lokedi, na Caroline Rotich, wote kutoka Kenya, wako katika orodha ya watakaowania tuzo ya Sh1.1 milioni.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending