Watu wawili wameangamia kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha malori mawili kwenye barabara ya Naivasha- Mai Mahiu.
Miili ya madereva wawili wa trela na lori waliohusika kwenye ajali hiyo ilikwama ndani ya vifusi vya magari hayo kwa takriban nusu saa kabla ya polisi kuwasili kuiondoa.
Lori lililohusika kwenye ajali. Picha: The Standard. Source: UGC
Ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la kibiashara la Longonot wakati dereva wa trela aliyekuwa akielekea Naivasha kuligonga lori liliokuwa upande wa pili.
Madera wa magari hayo walipoteza maisha yao papo hapo na kuwaacha wakaazi waking’ang’ania mchele uliokuwa ukisafirishwa na trela hiyo.