[ad_1]
Watu 2 wafariki baada ya gari lao kutumbukia mtoni
NA GEORGE MUNENE
WATU wawili akiwemo dereva Jumatatu waliaga dunia, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mto Rubingazi, katika daraja la Mwiria, kaunti ya Embu.
Mwanamke aliyekuwa abiria wa tatu katika gari hilo la Probox, aliokolewa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Embu.
“Tumemwokoa mwanamke aliyekuwa akisafiri katika gari lililopata ajali pekee. Tumeuopoa mwili mmoja na shughuli za kutafuta mwili wa dereva zinaendelea,” alisema Mkuu wa polisi Embu kaskazini Bw Abdullahi Adan.
Ajali hiyo ilitokea dereva aliposhindwa kudhibiti gari wakati wa kukata kona na likatumbukia majini.
Wakazi walilaumu serikali ya kaunti ya Embu kwa kutoweka vikingi kwenye daraja hilo ambapo ajali hiyo ilitokea.
[ad_2]
Source link