Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa watu wengine 257 wamepatikana na virusi vya COVID-19 na kufanya jumla ya idadi ya walioambukizwa virusi hivyo kufikia 8,528
Akizungumza akiwa kaunti ya Makueni Jumatano, Julai 8, Kagwe alisema visa hivyo vilipatikana baada ya sampuli kutoka kwa watu 3,053 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita.
Kufikia sasa, jumla ya sampuli zilizofanyiwa vipimo kote nchini ni 196,508.
Aidha, Kagwe alisema watu 2,593 wamepona kwa jumla baada ya wengine 89 kuruhusiwa kondoka hospitalini.
Watu waliofariki dunia kutokana na COVID-19 imefikia 169.
” Wagonjwa wawili wamefariki kutokana na ugonjwa huu, kwa sasa vifo 169 vimeripotiwa nchini, natuma rambi rambi zangu kwa familia zilizofiwa, ugonjwa huu kwa sasa umekita kambi katika jamii, kaunti zote isipokuwa 5 pekee zimeripoti visa vya maambukizi ya COVID-19, Lazima tuwe macho na tuchukue tahadhari zinazohitajka ili kudhibiti kueneea kwa ugonjwa huu,” Alisema Kagwe.
Kagwe pia amewasihi Wakenya hasa wanoishi jijini Nairobi wasitishe safari za kwenda mashinani kwani huenda wakasambaza virusi hivyo au wakaambukizwa.
Waziri huyo pia alifichua kuwa tangu Machi 13, wahudumu 257 wa afya wameambukizwa virusi hivyo wakiwa zamuni.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.