Watoto wawili wenye umri wa miaka 6 katika kijiji cha Kiptere wanauguza majeraha mabaya katika hospitali ya Sigowet baada ya kushambuliwa na jamaa mmoja aliyewakashifu kwa kumuibia mahindi
Chifu wa kata ndogo ya Kiptere David Kipkurui amethibitisha kisa hicho na amesema jamaa huyo aliyetambulika kwa majina kama Robert Chepkwony atachukuliwa hatua za kisheria.
Kulingana na ripoti za kuaminika, Chepkowny aliwapeleka vijana hao kwenye nyumba yake na kisha kuwakatakata kwa kisu akidai ni njia moja ya kuwaadhibu.
Inasemekana majirani waliosikia nduru nyumbani kwa mshukiwa waliwapata watoto hao wakiwa wamelala sakafuni huku damu ikitiririka.
Baada ya kutekeleza kitendo hicho cha unyama, mshukiwa alijaribu kutoroka ila alikamatwa na wakazi waliompeleka katika kituo cha polisi cha Sondu ambapo anazuiliwa kwa sasa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.