[ad_1]
Wazee wakemea wanasiasa wa UDA ‘kutusi’ Rais Kenyatta
NA STEPHEN MUNYIRI
KUNDI la viongozi kutoka eneobunge la Mathira, Kaunti ya Nyeri, limeshutumu baadhi ya wanasiasa wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) kwa ‘kumdharau’ Rais Uhuru Kenyatta.
Kundi hilo linadai kuwa wanasiasa hao wamekuwa wakimkosea heshima Rais Kenyatta kwa kuitusi familia yake.
Viongozi hao waliojumuisha wanachama wa Shirika la Maendeleo ya Wanawake (MYWO) na wazee wa Kiama Kiama kutoka maeneo ya Mathira Mashariki na Magharibi, walisema kuwa matusi hayo dhidi ya kiongozi wa nchi yanasababisha mgawanyiko nchini.
Mwenyekiti wa MYWO wa eneo hilo, Bi Grace Nyambura, aliwataka wanasiasa kuheshimu Rais hata kama hawakubaliani na msimamo wake wa kisiasa.
“Inasikitisha sana kuona baadhi ya viongozi wa kisiasa wakitusi Mama Ngina ambaye mume wake alipigania nchi na hata alikuwa rais wa kwanza wa Kenya,” akasema Bi Nyambura.
Mzee Muriithi Mutero mwanachama wa Kiama Kiama, kikundi cha kitamaduni cha jamii ya Wakikuyu, aliwataka viongozi wa kisiasa kuwa katika mstari wa mbele kuhubiri amani kote nchini.
Next article
Kilio uhaba wa mafuta ukiendelea
[ad_2]
Source link