Connect with us

General News

Waziri James Macharia asije akasahau kuwa mnamo Aprili 30, 2016 aliagiza kuwa ujenzi wa majengo ya orofa sharti uidhinishwe na NCA – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Waziri James Macharia asije akasahau kuwa mnamo Aprili 30, 2016 aliagiza kuwa ujenzi wa majengo ya orofa sharti uidhinishwe na NCA – Taifa Leo

TUSIJE TUKASAHAU: Waziri James Macharia asije akasahau kuwa mnamo Aprili 30, 2016 aliagiza kuwa ujenzi wa majengo ya orofa sharti uidhinishwe na NCA

WAPANGAJI katika jumba la orofa nne katika eneo la Kikuyu, kaunti ya Kiambu Jumamosi usiku, waliponea kifo kwa tundu la sindano, baada jengo moja lililokuwa likijengwa kuporomoka na kuangukia jumba hilo.

Duru zilisema kuwa jengo lililoporomoka halikuwa limekaguliwa na maafisa kutoka Mamlaka ya Kitaifa ya Majengo (NCA), ili kubainika kuwa salama.

Lakini Waziri wa Uchukuzi, Miundo Msingi na Ustawi wa Miji , Bw James Macharia, anayesimamia sekta hii, asije akasahau kuwa mnamo Aprili 30, 2016 aliagiza kuwa ujenzi wa majengo ya orofa sharti uidhinishwe na mamlaka hiyo.

Aliamuru mamlaka hiyo kubomoa majengo yote nchini ambayo yamejengwa bila idhini yake ili kuzuia maafa na hasara inayotokana na visa vya kuporomoka kwa majengo mabovu.

Kukithiri kwa visa vya kuporomoka kwa majengo, kunaonyesha amri ya Waziri Macharia imepuuzwa na maafisa wahusika.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending