Connect with us

General News

Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Amadou Gon Coulibaly afariki dunia

Published

on

– Amadou Gon Coulibaly aliaga dunia siku ya Jumatano, Julai 8, siku chache baada ya kurejea nyumbani akitokea Ufaransa kwa matibabu

– Alikuwa Waziri Mkuu wa Ivory Coast na mmoja wa wagombeaji wa urais kwa uchaguzi wa Oktoba 2020

– Gon mwenye miaka 61 ambaye alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 2012, alianza kuugua wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri na kupelekwa hospitalini ambapo alifariki

– Kifo chake kinaibua hali ya wasiwasi kuhusu uchaguzi nchini Ivory Coast

Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Amadou Gon Coulibaly aliaga dunia siku ya Jumatano, Julai 8, baada ya kuhudhuria mkutano wa mawaziri.

Kiongozi huyo mwenye miaka 61, alifariki miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais Oktoba 2020, ambapo alikuwa anagombea kiti hicho kupitia chama tawala cha RHDP.

Waziri Mkuu

Amadou Gon Coulibaly aliaga dunia siku ya Jumatano, Julai 8.

Kifo chake kilithibitishwa na Katibu Mkuu wa Rais wa Ivory Coast, Patrick Achi kupitia shirika la habari la serikali.

“Ninasikitika kutangaza kuwa Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly, mkuu wa serikali, alituacha mapema mchana wa leo baada ya kuhudhuria mkutano wa mawaziri,” alisema Achi.

Maafisa wanasema Coulibaly alianza kuugua wakati wa mkutano wa mawaziri katika Ikulu ya rais eneo la Abidjan na alikimbizwa hospitalini ambapo alikata roho.

Hata hivyo, haijabainika wazi namna Coulibaly alifariki.

Kiongozi huyo alirejea katika taifa hilo la Afrika Magharibi wiki jana baada ya miezi miwili nchini Ufaransa akipokea matibabu kutokana na matatizo ya moyo.

Coulibaly alihudumu kama waziri mkuu tangu Januari 2017 baada ya kuhudumu kama katibu mkuu wa rais kwa miaka sita.

Kifo chake kinaibua wasiwasi kuhusu uchaguzi nchini Ivory Coast ambapo hali ya kawaida ilikuwa imeanza kurejea baada ya miaka kadhaa ya migororo ya kisiasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Coulibaly aliteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama kinachoongozwa na Alassane Ouattara mapema Machi 2020, baada ya rais huyo kutangaza kuwa hatasimama tena kwa muhula wa tatu.

Ouattara alimuondoa aliyekuwa rais mwaka 2011, Laurent Gbagbo, ambaye alikataa kuondoka mamlakani baada ya kushindwa uchaguzi katika hali ambayo ilichochea vita na kupelekea watu 3,000 kupoteza maisha yao..

Waziri Mkuu

Coulibaly aliteuliwa kuwa mgombea wa urais wa chama kinachoongozwa na Alassane Ouattara.

Amehudumu kwa muhula miwili.

Kifo cha Coulibaly kinaibua maswali ya nani atachaguliwa kupeperusha bendera ya chama hicho.

Ni baba ya watoto watano ambaye alifuzu na shahada ya uhandisi nchini Ufaransa na kuwacha historia ya kuwa mtu mwenye bidii na hasira,

Hii ilimpeleka kubandikwa jina la utani la The Lion of Korhogo, ambapo ni mji mkuu wa taifa hilo.

Comments

comments

Trending