-Wendy Muthoni ambaye alikuwa anasomea Sheria katika chuo kikuu cha JKUAT tawi la Karen, alipumua pumzi yake ya mwisho katika Hospitali ya Nairobi
-Rais Uhuru alituma salamu zake za rambi rambi kwa familia ya Waziri wa Maji Sicily Kariuki na kuwaombea nguvu
-Ruto alisema marehemu atakumbukwa kwa ukarimu wake na kuwa mtu wa kutegemewa
Binti ya Waziri wa Maji, Sicily Kariuki, Wendy Muthoni ameaga dunia.
Muthoni, ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa sheria katika chuo kikuu cha JKUAT tawi la Karen, alifariki dunia katika Hospitali ya Nairobi lakini chanzo cha kifo chake hakijatajwa.
Katika taarifa kutoka Ikulu Jumapili, Julai 19 jioni, Rais Uhuru Kenyatta alituma salamu zake za rambi rambi kwa familia ya Waziri wa Maji Sicily Kariuki na kuwaombea nguvu
“Rais aliwatakia nguvu za Mwenyezi Mungu wakati huu mgumu wa kuomboleza na kuwahakikishia atasimama nao wakati wanakumbana na hali hiyo ya majonzi,” ilisoma taarifa hiyo.
Naibu Rais William Ruto alimtaja Muthoni kama mtu mwaminifu ambaye atakumbukwa kwa ukarimu wake na tegemeo.
“Pole zetu na maombi kwa familia ya Waziri Wa Maji, Sicily Kariuki kufuatia kifo cha binti yake mpendwa Wendy Muthoni ‘Noni’,” Ruto alisema.
Wakenya pia walijiunga pamoja na viongozi hao wawili kumuomboleza Muthoni huku wengi wakiombia familia hiyo utulivu.
Hii hapa baadhi ya jumbe zao za rambi rambi:
Kifo cha Muthoni kinakujia wakati taifa bado linamuomboleza muigizaji maarufu wa Citizen TV, Charles Bukeko, almaarufu Papa Shirandula.
Shirandula aliaga dunia katika hospitali ya Karen asubuhi ya Jumamosi, Julai 19, ambapo alikuwa amekimbizwa kwa matibabu baada ya kukumbana na matatizo ya kupumua.
Mwili wake ulisafirishwa kutoka jijini Nairobi mapema hii leo kuelekea Busia kwa mazishi siku ya Jumatatu, Julai 20.