Connect with us

General News

Wengi waliokosa kufanya KCPE watoka Nairobi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wengi waliokosa kufanya KCPE watoka Nairobi – Taifa Leo

Wengi waliokosa kufanya KCPE watoka Nairobi

Na FAITH NYAMAI

KAUNTI za Nairobi, Bungoma, Nakuru, Meru na Turkana ndizo zilirekodi idadi kubwa ya watahiniwa ambao hawakufanya Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) ambao matokeo yake yalitangazwa Jumatatu.

Mwaka huu, jumla ya wanafunzi 11,523 hawakufanya mtihani wao. Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa 863, huku Bungoma ikirekodi watahiniwa 682 ambao hawakufanya mtihani wa Darasa la Nane.

Nakuru ilirekodi watahiniwa 561, Meru 644, Turkana 589, Kakamega 583 na Trans Nzoia 524.

Kaunti zingine zilizorekodi idadi kubwa ya watahiniwa waliokosa kufanya KCPE ni pamoja na: Migori 362, Kilifi 316, Nyandarua 224, Muranga 232, Kiambu 331 Machakos 264, Kitui 315, Pokot Magharibi 454, Uasin Gishu 226, Narok 216, Busia 264, Kisumu 256, Kisii 231, Homabay 345, Siaya 239, na Kisumu 307.

Idadi hii kubwa ya wanafunzi ambao hawakufanya KCPE licha ya kujisajili imeibua hofu kwa Waziri wa Elimu Profesa George Magoha ambaye anakisia kuwa labda baadhi ya shule hizo zinawasajili wanafunzi hewa ili kusaidia katika wizi wa mtihani.

“Tunataka kupunguza idadi ya watahiniwa wanaokosa kufanya KCPE,” akasema waziri alipokuwa akitangaza matokeo.

Kaunti zilizorekodi idadi ndogo ya watahiniwa waliokosa kufanya mtihani wao ni pamoja na Wajir 40, Mandera 90, Nyamira 78, Elgeyo Marakwet 58, Bomet 86, Kericho 85, Samburu 63 na Tharaka Nithi 68.

Hata ingawa idadi ya watahiniwa waliokosa kufanya KCPE ilipungua kwa 12,424 ikilinganishwa na mwaka jana, kaunti zilizorekodi idadi kubwa 2020 zilisalia hivyo 2021.

Mwaka jana, Nairobi ilirekodi wanafunzi 1105 waliokosa kufanya KCPE wakifuatiwa na Migori kwa 462, Bungoma 480, Nakuru 472, Kakamega 453 na Turkana 429. Katika ripoti ya Prof Magoha, visa 320 vya wizi viliripotiwa huku waliohusika wakikamatwa.

Kaunti ya Kisumu ilirekodi idadi kubwa ya watahiniwa 49 waliofanya mtihani wao jelani huku Kakamega ikirekodi 39. Kaunti ya Kisii ilkuwa na watahiniwa 19, Bungoma 16, Siaya 15 na Narok 7.

Kaunti za Mombasa, Meru, Isiolo, Tharaka Nithi, Nairobi, Uasin Gishu, Busia, Bungoma, Kakamega, Vihiga, Kisumu na Siaya zilirekodi idadi kubwa ya watahiniwa wanawake ikilinganishwa na wanaume.

Idadi ya watahiniwa waliosajiliwa na ambao walikuwa wenye umri wa miaka 12 kwenda chini waliongezeka kutoka 26,378 mwaka jana hadi 33,627.

Kaunti hizo ni pamoja na Baringo 1,302, Bomet 1,932, Kericho 1,846, Pokot Magharibi 947 na Nyamira 1,111.

Kaunti zilizokuwa na watahiniwa waliokuwa na umri wa miaka 19 kwenda juu zilikuwa Turkana 2,755, Garissa 1,484, Kilifi 3,304, Kwale 1,904 na Mandera 386.

Watahiniwa 1,214,031 walifanya mtihani wao katika vituo 28,313 mwaka huu ikilinganishwa na 1,179,192 waliofanya 2020.

Hata hivyo, watahiniwa 1,225,507 walikuwa wamejisajili ili kufanya mtihani wa KCPE mwaka huu.